Makala mpya za kilimo, ufugaji na teknolojia
Mkulima, kilimo cha pamba ni biashara inayoweza kukupa kipato kizuri ikiwa utaisimamia kwa wakati na kwa kufuata kanuni sahihi za kilimo. Pamba si zao la kupanda na kuliacha shambani mpaka wakati wa kuvuna. Tunahitaji kuanza na uchaguzi sahihi wa shamba, mbegu bora, muda sahihi wa kupanda, nafasi sahihi, lishe ya mmea, udhibiti wa magugu, ufuatiliaji wa wadudu na magonjwa, pamoja na uvunaji na utunzaji sahihi wa pamba baada ya kuvuna.