Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Majibu ya maswali ya kawaida kuhusu bidhaa na huduma zetu
Je, naweza kuagiza bidhaa nikiwa mkoa mwingine?
Ndiyo! Tunafikisha bidhaa Tanzania nzima. Weka oda kupitia tovuti, WhatsApp au simu, na timu yetu itapanga usafirishaji kupitia mabasi au wasafirishaji wa mizigo. Kwa kawaida bidhaa hufika ndani ya siku 2–5 za kazi.
Nitalipaje bidhaa ninazoagiza?
Unaweza kulipa kwa njia mbili: Malipo wakati wa kupokea (Cash on Delivery) — lipa fedha taslimu au kwa simu unapopokea bidhaa; au malipo ya mtandaoni kupitia Selcom — M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa au kadi ya benki.
Je, bidhaa zenu ni halisi (original)?
Ndiyo. Tunanunua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji na mawakala rasmi waliosajiliwa na TPRI/TFDA. Kila bidhaa ina lebo halisi ya mtengenezaji na maelekezo kamili ya matumizi.
Sijui dawa gani inafaa kwa tatizo la shamba langu. Mnaweza kunisaidia?
Bila shaka! Tuma picha za tatizo (majani, wadudu, ugonjwa) kwa WhatsApp +255 741 348 284 au tumia Msaidizi wetu wa AI kwenye tovuti. Wataalamu wetu watakushauri dawa sahihi, kipimo na jinsi ya kutumia — bure kabisa.
Je, mnauza kwa bei ya jumla kwa vikundi na mashamba makubwa?
Ndiyo, tuna bei maalum za jumla kwa vikundi vya wakulima, vyama vya ushirika, mashamba makubwa na wauzaji wadogo (retailers). Wasiliana nasi moja kwa moja kupata orodha ya bei za jumla.
Naweza kurudisha bidhaa niliyonunua?
Bidhaa ambazo hazijafunguliwa zinaweza kurudishwa ndani ya siku 7 kama zina kasoro ya kiwandani au ulipokea bidhaa tofauti na uliyoagiza. Kwa sababu za usalama, dawa zilizofunguliwa hazirudishwi. Soma Sera yetu ya Marejesho kwa maelezo kamili.
Mko wapi na mnafunguliwa saa ngapi?
Duka letu kuu lipo Mbuyuni-Manyema, Moshi Mjini, Kilimanjaro. Pia tuna tawi la Lushoto Agro Inputs mkoani Tanga. Tunafunguliwa Jumatatu hadi Jumamosi, saa 1:30 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (7:30 AM – 6:00 PM).
Je, mnatoa mafunzo au ushauri wa kilimo?
Ndiyo. Ushauri wa kitaalamu ni bure kwa wateja wote — dukani, kwa simu au WhatsApp. Pia tunaendesha mafunzo ya vikundi na kutembelea mashamba. Angalia ukurasa wa Huduma Zetu.
Hukupata jibu lako?
Chat kwa WhatsApp