+255 741 348 284
|
CHETU AGROSOLUTION logo

Sera ya Faragha

CHETU AGROSOLUTION Co. Ltd ("sisi") inaheshimu faragha yako. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako unapotumia tovuti yetu chetuagro.com.

Taarifa Tunazokusanya

  • Taarifa unazotupatia: jina, namba ya simu, barua pepe, anuani ya usafirishaji, taarifa za shamba (kwa usajili wa wakulima) na ujumbe unaotutumia.
  • Taarifa za oda: bidhaa ulizonunua, kiasi na njia ya malipo. Hatuhifadhi namba za kadi au PIN za simu — malipo ya mtandaoni yanashughulikiwa na Selcom.
  • Taarifa za kiufundi: IP address na taarifa za kivinjari kwa ajili ya usalama.

Jinsi Tunavyotumia Taarifa

  • Kushughulikia oda zako na kukufikishia bidhaa.
  • Kukupa huduma kwa wateja na ushauri wa kitaalamu.
  • Kukutumia taarifa za bidhaa, ofa na elimu ya kilimo — endapo umekubali.
  • Kuboresha huduma zetu na usalama wa tovuti.

Kushirikisha Taarifa

Hatuuzi taarifa zako. Tunashirikisha taarifa na watoa huduma wanaotusaidia kuendesha biashara tu — kama Selcom (malipo) na makampuni ya usafirishaji — na pale sheria inapotaka.

Usalama na Uhifadhi

Taarifa zako zinahifadhiwa kwenye mifumo salama iliyolindwa. Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako wakati wowote kwa kuwasiliana nasi: info@chetuagro.com au +255 741 348 284.