+255 741 348 284
|
CHETU AGROSOLUTION logo
nyanya

Blossom End Rot

18 Septemba 2026

Blossom End Rot

Blossom End Rot (BER) ni tatizo linalotokea sana kwenye nyanya, pilipili na baadhi ya mazao mengine, ambapo sehemu ya chini ya tunda inapokuwa imekabiliana na ua hubadilika kuwa kahawia au nyeusi, kisha hukauka na kuzama.

Sababu kuu

  • Upatikanaji hafifu wa calcium kwenye tunda — mara nyingi si kwa sababu udongo hauna calcium, bali mmea hauwezi kuifikisha vizuri kwenye tunda.
  • Mabadiliko makubwa ya unyevu wa udongo — kukauka sana kisha kupata maji mengi.
  • Ukuaji wa mmea kwa kasi sana.
  • Mizizi kuharibika au udongo kuwa na tatizo la mizizi.

Jinsi ya kudhibiti

  1. Mwagilia kwa utaratibu ili udongo uwe na unyevu unaofanana.
  2. Tumia matandazo (mulch) kusaidia kuhifadhi unyevu.
  3. Epuka kumwagilia kwa wingi baada ya mmea kukaa muda mrefu bila maji.
  4. Fanya soil test ili kujua kiwango cha calcium na pH ya udongo.
  5. Hakikisha mizizi ina afya na udongo una drainage nzuri.
  6. Epuka matumizi ya mbolea nyingi za nitrogen, hasa zinazosababisha ukuaji wa majani kwa kasi.

Muhimu: Blossom end rot si ugonjwa unaoambukizwa kutoka mmea mmoja kwenda mwingine. Ni tatizo la kifizikia linalohusishwa zaidi na usafirishaji wa calcium na usimamizi wa maji.

Sambaza:

Makala za Karibuni

Angalia Zote