+255 741 348 284
|
CHETU AGROSOLUTION logo
soil, udongo, afya ya udongo

Upimaji wa Afya ya Udongo

20 Septemba 2026

Upimaji wa Afya ya Udongo

Upimaji wa afya ya udongo ni mchakato wa kuchunguza hali ya udongo ili kujua kiwango cha rutuba, virutubisho, pH, unyevu, pamoja na uwezo wake wa kusaidia ukuaji mzuri wa mimea.

Vipimo muhimu vya afya ya udongo

  1. pH ya udongo – huonyesha kama udongo una tindikali nyingi au una alkali.
  2. Virutubisho – hupima virutubisho muhimu kama Nitrojeni (N), Fosforasi (P) na Potasiamu (K), pamoja na virutubisho vingine.
  3. Kaboni hai (Organic Matter) – huonyesha kiasi cha mabaki ya viumbe hai yanayosaidia kuboresha muundo na rutuba ya udongo.
  4. Muundo wa udongo – huangalia uwiano wa mchanga, tifutifu na mfinyanzi.
  5. Unyevu na uwezo wa kuhifadhi maji – husaidia kujua jinsi udongo unavyoweza kuhifadhi maji kwa ajili ya mimea.
  6. Viumbe hai wa udongo – minyoo na vijidudu husaidia katika mzunguko wa virutubisho na uboreshaji wa udongo.

Kwa nini upime udongo?
Upimaji husaidia mkulima kufanya maamuzi sahihi kuhusu aina na kiasi cha mbolea, chokaa inapohitajika, umwagiliaji na uchaguzi wa mazao. Hivyo, unaweza kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza afya ya udongo na uzalishaji wa mazao.

Sambaza:

Makala za Karibuni

Angalia Zote