Kilimo cha Vitunguu Maji: Hatua kwa Hatua
Na CHETU AGROSOLUTION · 18 Julai 2026

Vitunguu maji vina soko kubwa Tanzania na nchi jirani. Zao hili huchukua miezi 4–5 kutoka kupanda hadi kuvuna, na huhitaji mipango mizuri.
1. Kitalu (Siku 1–45)
Sia mbegu kwenye matuta ya kitalu yenye udongo laini uliochanganywa na mboji. Mwagilia kwa wastani kila siku. Miche huwa tayari baada ya siku 40–45 ikiwa na unene wa penseli.
2. Kuandaa Shamba na Kupandikiza
- Lima na laini udongo vizuri; vitunguu vinapenda udongo tifutifu usiotuamisha maji.
- Weka mbolea ya kupandia yenye fosforasi (DAP au NPK).
- Pandikiza kwa nafasi: sentimita 30 kati ya mistari, sentimita 8–10 kati ya mimea.
3. Palizi na Mbolea ya Kukuzia
Vitunguu havishindani vizuri na magugu — palilia mapema na mara kwa mara. Wiki 3–4 baada ya kupandikiza weka mbolea ya kukuzia (CAN au UREA kwa kipimo), rudia wiki 3 baadaye.
4. Magonjwa na Wadudu
- Purple blotch na downy mildew: piga fungicide za kinga hasa hali ya unyevu.
- Thrips: wadudu wadogo wanaokausha majani — dhibiti mapema.
5. Kuvuna na Kuhifadhi
Vuna majani yakianza kulala na kukauka (asilimia 50–70 ya shamba). Anika vitunguu kivulini siku 7–14 mpaka shingo zikauke kabisa. Hifadhi mahali penye hewa ya kutosha — vitunguu vilivyokaushwa vizuri hukaa miezi 3–6, ukisubiri bei nzuri.
Tuna mbegu bora za vitunguu, mbolea na dawa. Nunua hapa au uliza ushauri bure.


